Friday, December 19, 2014

TUNAWEZAJE KUOKOLEWA NA UHARIBIFU ULIOKO DUNIANI

Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa. 2 Pet 1:4

1.Tumekirimiwa ahadi kubwa mno za thamani
2.tupate tabia ya Uungu
tabia hiyo itatuwezesha kuokolewa na uharibifu huo

Monday, December 1, 2014

LETA USHAWISHI KATIKA UFALME

Kulikuwa na semina jmosi tar 29/11/2014 inayohusu "kuendesha biashara inayoleta ushawishi katika ufalme wa Mungu".Nimejifunza mengi sana katika semina hiyo.

1.Ni muhimu sana kuwa na mtazamo sahihi(kuhusu unalotaka kufanya) tunapotaka kufanya bishara au kitu kingine.Katika biashara mimi kama Mkristo ninapaswa kuingia katika biashara nikiwa ni mtazamo unaolenga kwanza kuhusu ufalme wa Mungu mfano: sipaswi kuingia katika biashara kutafuta faida tu,kwanza nilenge kutumia bishara yangu kuhudumia jamii kwa namna mbalimbali mfano kwa kuboresha maisha ya watu,kutatua matatizo ya jamii husika na pia kuufanya ufalme wa Mungu uje katika mahali nilipo.Tutakapokuwa na mtazamo huo hata mtaji,wateja havitakuwa kazi kwetu,Mungu mwenyewe atashughulika na hayo maana ndivyo alivyosema katika Neno lake "Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu,na haki yake na mengine yote mtazidishiwa".

Tunapaswa kufahamu kuwa sisi sio wamiliki wakuu wa biashara zetu.Kwa kuwa sisi ni mali ya Mungu,mmiliki mkuu wa biashara zetu ni Mungu,Tumkabidhi Yeye ili azitumie kwa utukufu wa Jina lake.

Mungu ametupa vipawa,ujuzi mbalimbali.Tunapaswa kuvitumia tukijua si mali yetu bali tumepewa dhamana na tutaulizwa tulivitumiaje kama mifano wa wale waliopewa talanta kwenye Biblia.

2. Kila Mtu ana vitu kwa ajili ya kizazi chake.Tumezaliwa navyo,kwa hiyo tusijidharau,tujitambue na kuwa na ujasiri wa kuanza kuvitumia kwa ajili ya utukufu wa Mungu.Tumezaliwa na suluhisho la matatizo mbalimbali.Tusilalamikie matatizo bali tutumie hayo kama changamoto ya kutusaidia kujua na kukuza vipaji vyetu.Je kwenye jamii inayokuzunguka unaona kuna mapungufu gani?unadhani unaweza kufanya nini kusaidia katika hayo?kumbuka wewe Mkristo ni nuru,wewe ni Chumvi unapaswa kuangaza.Jitambue,mshirikishe Mungu katika maisha yako umruhusu atawale kweli na kwa pamoja naye utaweza kutambua ulivyonavyo na kuleta ushawishi katika ulimwengu unaokuzunguka.


"Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake" Yoh 4:34

Mungu Mwema atubariki sote tunapoendelea kuyatafuta mapenzi yake katika yote .AMEN.