Monday, September 28, 2015

Sheria,amri na maagizo ya Bwana

7Sheria ya Bwana ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa Bwana ni amini, Humtia mjinga hekima.
8 Maagizo ya Bwana ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya Bwana ni safi, Huyatia macho nuru.
9 Kicho cha Bwana ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za Bwana ni kweli, Zina haki kabisa.
10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
11 Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi.
12 Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri.
13 Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa.
14 Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. Zab 19:7-14

Monday, February 16, 2015

NIENDAVYO KWARESMA HII(nataka kuwa chumvi ya ulimwengu)


Habari wapendwa!

Jumatano tar 18/02/2015 ni siku tunayoanza mafungo katika Kwaresma.
Kila mwaka huwa tunafanya hivi,mwaka huu naona Mungu anasema nami kwa namna ya tofauti kwa habari ya malengo ya mafungo ya mwaka huu.

Nimejikuta natamani sana mwaka huu mafungo yangu yalenge hasa katika eneo la utumishi.Natamani Mungu anitengeneze na aseme nami kwa kina kuhusu utumishi na huduma aliyoniitia.Ninategemea kufanya yafuatayo kama sehemu ya mafungo yangu:

1.Kupata muda wa kutosha kuomba kwa kina sana.
2.Kusoma kwa bidii na kwa kina Neno la Mungu
3.Kuchochea karama yangu kwa maana ya kufanya kile kinochohusiana na karama yangu ili nipate kujifunza zaidi.

Ninakualika na wewe mwenzangu,eneo ambalo unaona Mungu anasema nawe likae sawa na bado unaona hujaweza kulitendea haki,fanya kitu kwaresma hii.

Ni maombi yangu kwa Mungu kwamba Kipindi hiki kisipite bure bali tuvuke kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa utukufu wa Jina lake.Vile viwango ambavyo tumekuwa tunatamani kuvifikia tumsihi Mungu  atufikishe hapo kwaresma hii.
 
Ninamwomba Mungu kabla ya kuanza kwa mafungo hayo niweze kujiaandaa kikamilifu na anipe Neema ya pekee itakayoniwezesha kufanya mafungo hayo kwa ukamilifu na kwa namna  inakayompa yeye Mungu utukufu,AMEN.

**********nataka kuwa chumvi*********nataka kuwa chumvi *******


Monday, January 26, 2015

MAPENZI YA MUNGU

MAPENZI YA MUNGU- KUYAJUA NA KUYATENDA



KUYAJUA MAPENZI YAKE
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Rum 12:1-2

KUYATENDA MAPENZI YAKE
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.       1 Yoh 2:15-17