Monday, February 16, 2015

NIENDAVYO KWARESMA HII(nataka kuwa chumvi ya ulimwengu)


Habari wapendwa!

Jumatano tar 18/02/2015 ni siku tunayoanza mafungo katika Kwaresma.
Kila mwaka huwa tunafanya hivi,mwaka huu naona Mungu anasema nami kwa namna ya tofauti kwa habari ya malengo ya mafungo ya mwaka huu.

Nimejikuta natamani sana mwaka huu mafungo yangu yalenge hasa katika eneo la utumishi.Natamani Mungu anitengeneze na aseme nami kwa kina kuhusu utumishi na huduma aliyoniitia.Ninategemea kufanya yafuatayo kama sehemu ya mafungo yangu:

1.Kupata muda wa kutosha kuomba kwa kina sana.
2.Kusoma kwa bidii na kwa kina Neno la Mungu
3.Kuchochea karama yangu kwa maana ya kufanya kile kinochohusiana na karama yangu ili nipate kujifunza zaidi.

Ninakualika na wewe mwenzangu,eneo ambalo unaona Mungu anasema nawe likae sawa na bado unaona hujaweza kulitendea haki,fanya kitu kwaresma hii.

Ni maombi yangu kwa Mungu kwamba Kipindi hiki kisipite bure bali tuvuke kutoka eneo moja kwenda eneo lingine kwa utukufu wa Jina lake.Vile viwango ambavyo tumekuwa tunatamani kuvifikia tumsihi Mungu  atufikishe hapo kwaresma hii.
 
Ninamwomba Mungu kabla ya kuanza kwa mafungo hayo niweze kujiaandaa kikamilifu na anipe Neema ya pekee itakayoniwezesha kufanya mafungo hayo kwa ukamilifu na kwa namna  inakayompa yeye Mungu utukufu,AMEN.

**********nataka kuwa chumvi*********nataka kuwa chumvi *******


No comments:

Post a Comment