Thursday, July 19, 2012

UJUMBE J2 YA 14 MWAKA B

Mk 6:1-6
1.Tusimwangalie aletaye ujumbe pekee bali tupokee zaidi ujumbe utokao kwa Mungu
2.Tuangalie mambo kwa mitazamo ya kiroho si kimwili tu mfano tusidhani tumemfahamu Yesu tukashindwa kuona zaidi katika Roho



UJUMBE MKUTANO WA SALA WA VIJANA 01-07-2012

NAMNA/MBINU MBALIMBALI ZA KULIFANYIA KAZI NENO LA MUNGU
1.Kusoma Neno
2.Kutafakari Neno
3.Kusali Neno mfano kupitia Zaburi mbalimbali
4.Kujifunza Neno mfano kujifunza kuhusu Roho Mtakatifu,utoaji,baraka nk unapitia vifungu vinavyosema juu ya hayo unayotaka kujifunza
5.Kukariri Neno
6.Kutenda Neno
7.Kushirikisha Neno

Ni vizuri kutenga muda wa kutosha  kila siku,kwa wiki ,mwezi ili kutumia mbinu hizo.Tukifanya hayo kwa msaada wa  Roho Mtakatifu Mungu atabadilisha maisha yetu kwa Utukufu wake nasi tutafurahia maisha,tutaweza kumjua Mungu,kumpenda,kumtumikia na mwisho kufika kwake Mbinguni kama  yalivyokuwa makusudi yake Mungu ya kutuweka duniani.


UJUMBE MKUTANO WA SALA WA VIJANA 24-06-2012

NENO LA MUNGU
1.Neno la Mungu ni Chakula 1Pet2:2
2.Neno la Mungu ni Mbegu
3.Neno la Mungu ni Maji Isa 55:10
4.Neno la Mungu ni uponyaji/hutupa afya Mith 4:21
5.Neno la Mungu hutupa ushindi dhidi ya dhambi Zab 119:11
6.Neno la Mungu hutupa  ushindi katika majaribu Zab 120


Monday, June 11, 2012

UJUMBE SIKUKUU YA EKARISTI

Ikiwa jana ilikuwa ni sikukuu ya Ekaristi Takatifu,ningependa kuwashirikisha yaliyofundishwa nilipohudhuria ibada ya misa kigango cha Kiseke Parokia ya Ilemela.

Ujumbe wa jumapili sikukuu ya Ekaristi Takatifu.
Tunapompokea Yesu wa Ekaristi tunapaswa kufanana nae.
Swali la kujiuliza: kwa nini tunampokea Yesu mara kwa mara lakini hatubadiliki?bado tunapenda dhambi?tunafanya mambo yetu wenyewe badala ya kufanya yale anayotaka Mungu kama Yesu alivyokuwa anafanya?

Jibu:
1.Hatuna Imani ya Kutosha kwa Yesu
2.Hatujaamini uwepo wa Yesu katika Ekaristi Takatifu

Yatupasayo
Inatupasa tumwombe Mungu atuongezee imani kwake na kwa Yesu Kristo mwanae.
Mara tutakapokuwa na Imani ya Kutosha (kubwa na thabiti) kwa Yesu na kuamini uwepo wake katika Ekaristi Takatifu,tutamwabudu inavyopasa na kumpokea kwa heshima na Uchaji mkubwa.
Yesu atakapokuwa ameingia katika maisha yetu atayabadilisha yafanane naye na hivyo hatutakuwa tena sisi tunaishi bali Kristo ndani yetu ndiye atakuwa akiishi katika maisha yetu.


Wito
Ekaristi Takatifu inatupatia neema nyingi sana tunazozihitaji katika maisha yetu.Neema ni msaada wa Mungu utuwezeshao kutenda mema.Tumkaribishe basi  Yesu wa Ekaristi mioyoni mwetu kwa kupokea Ekaristi Takatifu katika hali ya usafi mara kwa mara  ili atujaze neema nyingi zitakazotusaidia kumpendeza Mungu katika maisha yetu.

Baada ya kuwa tumemkaribisha Yesu katika mioyo yetu nakumruhusu atawale maisha yetu,tunapaswa kumshuhudia na kumtangaza kwa watu wote.



Friday, June 8, 2012

JUNE PRAYER POINTS

Baadhi ya mambo ya kuombea mwezi huu

VIJANA
-Vijana tupate maono kutoka kwa Mungu kupitia Roho wake Mtakatifu (Mdo 2:14-18 )
-Maono yote Mungu aliyokwishatupa yakapate kutimia kwa wakati wake,Mungu afanye njia sawa sawa na Zab 33:10-11 (yataje hapa maono hayo)
-Nguvu ya Ujana itumike kumtukuza Mungu (1 Yoh 2:13-14)



KANISA
-Roho ya Hekima na Ufunuo katika kumjua Mungu (Ephe 1:17)
-Kumpenda Mungu na kumheshimu Mungu kweli kweli
-Kanisa tufahamu mamlaka na nguvu alizotupa Kristo na kutenda kazi yake kwa ujasiri (Efe 1:18-23)
-Watendakazi katika shamba la Bwana waongezeke: Mungu aachilie karama na fadhila zake kwa wingi zaidi na zaidi

TAIFA
Roho ya Hekima  kwa viongozi
Moyo wa upendo  viongozi
Umoja,upendo na amani kwa watu wote

ISRAEL
-Favour na Kibali cha Mungu viendelee kuwa pamoja nao
-Zab 33:10-11

WATU WOTE
-Paji la Imani kwa Yesu Kristo kwa watu wote
-Tufahamu ukweli na ukweli utuweke huru kweli kweli Yoh 8:32
-Neema ya wokovu
-Maono yote Mungu aliyokwishatupa yakapate kutimia kwa wakati wake,Mungu afanye njia sawa sawa na Zab 33:10-11 (yataje hapa maono hayo)







MKUTANO WA SALA NYAKAHOJA

Alhamisi hii masomo yalikuwa

Zaburi (Psalms) 103:1-22
Kutoka (Exodus) 23:27
Yeremiah Jer 30:16

Mungu ametukumbusha upendo wake usivyo na mipaka katika zab 103

Pia ametukumbusha kumwomba daima ulinzi kupitia Neno lake. na si ulinzi tu bali kila tuombayo tuombe sawa sawa na Neno lake linavyotuahidi.