Thursday, July 19, 2012

UJUMBE J2 YA 14 MWAKA B

Mk 6:1-6
1.Tusimwangalie aletaye ujumbe pekee bali tupokee zaidi ujumbe utokao kwa Mungu
2.Tuangalie mambo kwa mitazamo ya kiroho si kimwili tu mfano tusidhani tumemfahamu Yesu tukashindwa kuona zaidi katika Roho



UJUMBE MKUTANO WA SALA WA VIJANA 01-07-2012

NAMNA/MBINU MBALIMBALI ZA KULIFANYIA KAZI NENO LA MUNGU
1.Kusoma Neno
2.Kutafakari Neno
3.Kusali Neno mfano kupitia Zaburi mbalimbali
4.Kujifunza Neno mfano kujifunza kuhusu Roho Mtakatifu,utoaji,baraka nk unapitia vifungu vinavyosema juu ya hayo unayotaka kujifunza
5.Kukariri Neno
6.Kutenda Neno
7.Kushirikisha Neno

Ni vizuri kutenga muda wa kutosha  kila siku,kwa wiki ,mwezi ili kutumia mbinu hizo.Tukifanya hayo kwa msaada wa  Roho Mtakatifu Mungu atabadilisha maisha yetu kwa Utukufu wake nasi tutafurahia maisha,tutaweza kumjua Mungu,kumpenda,kumtumikia na mwisho kufika kwake Mbinguni kama  yalivyokuwa makusudi yake Mungu ya kutuweka duniani.


UJUMBE MKUTANO WA SALA WA VIJANA 24-06-2012

NENO LA MUNGU
1.Neno la Mungu ni Chakula 1Pet2:2
2.Neno la Mungu ni Mbegu
3.Neno la Mungu ni Maji Isa 55:10
4.Neno la Mungu ni uponyaji/hutupa afya Mith 4:21
5.Neno la Mungu hutupa ushindi dhidi ya dhambi Zab 119:11
6.Neno la Mungu hutupa  ushindi katika majaribu Zab 120