Ikiwa jana ilikuwa ni sikukuu ya Ekaristi Takatifu,ningependa kuwashirikisha yaliyofundishwa nilipohudhuria ibada ya misa kigango cha Kiseke Parokia ya Ilemela.
Ujumbe wa jumapili sikukuu ya Ekaristi Takatifu.
Tunapompokea Yesu wa Ekaristi tunapaswa kufanana nae.
Swali la kujiuliza: kwa nini tunampokea Yesu mara kwa mara lakini hatubadiliki?bado tunapenda dhambi?tunafanya mambo yetu wenyewe badala ya kufanya yale anayotaka Mungu kama Yesu alivyokuwa anafanya?
Jibu:
1.Hatuna Imani ya Kutosha kwa Yesu
2.Hatujaamini uwepo wa Yesu katika Ekaristi Takatifu
Yatupasayo
Inatupasa tumwombe Mungu atuongezee imani kwake na kwa Yesu Kristo mwanae.
Mara
tutakapokuwa na Imani ya Kutosha (kubwa na thabiti) kwa Yesu na kuamini
uwepo wake katika Ekaristi Takatifu,tutamwabudu inavyopasa na kumpokea
kwa heshima na Uchaji mkubwa.
Yesu atakapokuwa ameingia katika
maisha yetu atayabadilisha yafanane naye na hivyo hatutakuwa tena sisi
tunaishi bali Kristo ndani yetu ndiye atakuwa akiishi katika maisha
yetu.
Wito
Ekaristi Takatifu inatupatia neema nyingi sana
tunazozihitaji katika maisha yetu.Neema ni msaada wa Mungu utuwezeshao
kutenda mema.Tumkaribishe basi Yesu wa Ekaristi mioyoni mwetu kwa
kupokea Ekaristi Takatifu katika hali ya usafi mara kwa mara ili
atujaze neema nyingi zitakazotusaidia kumpendeza Mungu katika maisha
yetu.
Baada ya kuwa tumemkaribisha Yesu katika mioyo yetu nakumruhusu atawale
maisha yetu,tunapaswa kumshuhudia na kumtangaza kwa watu wote.
No comments:
Post a Comment